Walifika Mlimani hoteli saa sita na nusu mchana. Wakati dereva huyo akitafuta mahali pa kuegesha gari, Jacob akatumia fursa hiyo kumwangalia na kuitalii sura yake. Alianza kuamini kuwa yawezekana akawa si dereva kama madereva wengine.
Haikumchukua muda mrefu sana kuona tofauti, baada ya kuanza uchunguzi wake kwa mzee huyu, Jacob aligundua kuwa alikuwa amevaa sura ya bandia usoni.
Mara hii hamu ya kutaka kujua mzee huyu alikuwa ni mtu wa namna gani iliongezeka huku ikichanganyikana na wasiwasi wa kuwa huenda mzee huyu alikuwa ametumwa makusudi kuja kumpokea.
Wakati anamaliza kuwaza hayo tayari mzee huyo alikuwa ameshaegesha gari na kusubiri abiria atoe ujira wake na kushuka. Baada ya kuwa ameshamlipa, Jacob alishuka kwa tahadhali kubwa maana mpaka hapo hakuwa anamwamini tena. Alianza kupiga hatua kuelekea ndani ya hoteli hii ya Mlimani.
Kama ungefanikiwa kumwona usingepeta taabu kugundua kuwa alikuwa katika vita ya mawazo. Mawazo mengine yalikuwa yakimtuma amfuatilie huyu mzee huku mengine yakigoma. Baada ya mjadala mkali ndani ya kichwa chake aliona kuwa mzee yule anaweza kuwa ni mtego, hivyo ni vema apoteze nyayo zake toka kwa yeyote aliyekuwa akijua juu ya ujio wake.
Alipofika mapokezi Mpelelezi Jacob Matata hakupata tatizo kupata chumba. Chumba alichopata kilikuwa orofa ya tatu namba 321. Ilimchukua dakika kadhaa mpaka pale alipouona mlango wa chumba alichokuwa amepewa. Kabla hajaingiza ufunguo kwenye kitasa cha mlango Jacob aliangalia ili kuona kama kuna mtu aliyekuwa anategemea au kusubiri kuona sura yake eneo hilo. Hakuona yeyote. Alingiza funguo katika kitasa na kuuzungusha, mlio uliotokea uliashiria kuwa mlango ulikuwa unasubiri mtu kuusukuma ili umruhusu aingie ndani. Jacob hakuusukuma wala hakuwa na haja ya kuingia ndani. Alichomoa ufunguo na kuanza kuondoka eneo hilo. Alipofika umbali fulani toka mlangoni hapo, alitafuta kona nzuri ya kuweza kujibanza.
Huku akijifanya kama anayemsubiri mtu fulani, alikuwa anasubiri kuona kama kuna mtu angekuja kuchunguza kile chumba. Dakika kadhaa zilipita bila kuwa na dalili yoyote ya mtu kuchunguza chumba hicho. Jacob hakuona sababu ya kuendelea kusubiri, hivyo kwa kupitia njia za kughushi aliweza kutoka ndani ya Mlimani hoteli.
Hapo nje alichukua taxi nyingine na kuomba apelekwe Paradiso hoteli. Hapo ndipo aliamua kuwa ndipo yangekuwa makazi yake kwa siku hiyo.

* * *
Baada ya kuoga na kupata kahawa katika mgahawa wa hoteli hii ya Paradiso, Jacob alijisikia vizuri hasa ukizingatia muda huo mji wa Arusha ulikuwa na baridi kali sana. Baada ya kupata kahawa hiyo alirudi chumbani kwake ili apange namna ya kuanza shughuli ya kuwasaka wanaopanga kufanya mambo ambayo kila mpenda amani angekuwa kinyume nao na inamaana alitakiwa kupambana na Max ‘the Fuse’.
Alipoona kila kitu kiko sawa, alijilaza kiandani huku akifikiria ni wapi pa kuanzia. Kila alipofikiria hakuona kama angepata msaada wa haraka wa kumpa japo dondoo za mambo alivyo ndani ya Arusha. Polisi ndiyo wangeweza kumpa taarifa za haraka, lakini tayari alikuwa ameshapewa taarifa za kuuwawa askari kadhaa ikiwa ni pamoja na Inspekta Sogoyo aliyeuawa masaa machache yaliyokuwa yamepita. Sababu nyingine ya kutotaka kuonana nao ni ileile ya kutotaka kujulikana kuwa yuko Arusha. Japo alijua fika kuwa Polisi wangefurahi sana kusikia kuwa mtu kama yeye yuko Arusha kwa kipindi kama hiki ambacho mji huu unawaka moto.

Asubuhi hii Jacob aliamka mapema sana, alitoka kitandani na kuwasha televisheni iliyokuwapo chumbani hapo. Aliangalia taarifa za habari na matukio kupitia vituo mbalimbali vya televisheni.
Jambo moja lililomfurahisha ni pale alipoona mwenyekiti wa mkutano ambao ulikuwa umepokea vitisho usifanyike, alisisitiza kuwa pamoja na yote yaliyokuwa yametokea Arusha lakini mkutano ni lazima uwepo. Pia alitoa wito kwa viongozi wote wa usalama wa nchi hizo kufanya jitihada zote kuhakikisha kuwa watu waliohusika na kutoa vitisho watafutwe na kukamatwa haraka iwezekanavyo.
Jacob alitoka kitandani na kufanya mazoezi kidogo chumbani humo katika hali ya kuweka mwili kuwa ‘fit’ zaidi. Baada ya hapo aliingia bafuni kuoga. Muda mfupi baadae alikuwa ameshamaliza usafi na kuvaa, hivyo akawa tayari kwa kuondoka. Wakati akiwa amesimama tayari kwa kuondoka, simu yake ya mkononi iliita. Aliipokea.
“Hallo nani na nikusaidie nini” Jacob aliuliza mara baada ya kubonyeza kitufe cha kupokelea.
“ Unaongea na Mzee Edson Kinyaro hapa. Naomba tuonane, niko nje ya hoteli uliyofikia sehemu ya kuegeshea magari. Utanikuta ndani ya gari aina ya Landrover Discover ya bluu” Alipomaliza kusema kama kawaida yake alikata simu.
Jacob akabaki na mshangao, alijiuliza ni namna gani mzee huyu alikuwa amejua kuwa alikuwa ameshakuja Arusha, kwani katika maongezi kwa njia ya simu wakati Jacob alipokuwa Dar hakukumbuka kuwa alimwambia kuwa angekuja Arusha. Sasa alijuaje kuwa Jacob tayari ameshafika na tena ni kwenye hoteli ya Paradiso baada ya kuikwepa ile ya Mlimani.
Ni kweli alikuwa anamfahamu sana mzee Edson, lakini taratibu za kazi hazimruhusu kuonana na watu wakubwa kama Edson katika uwanja wa mapambano. Edson ni hazina ya taifa kwani licha ya kuwa ameshastaafu lakini alikuwa na taarifa ambazo ni siri ya kiwango cha juu kwa taifa. Hivyo kwa mpelelezi kama yeye haikuwa vema kuhatarisha maisha ya mzee huyo kwa wakati ambao ameshahisi kuna kila dalili ya hatari katika mji wa Arusha. Pia alifikiria kuwa kwa vile yeye na Edson wanamjua Max, mara moja Max hatochelewa kuyaondoa maisha ya Edson kama akihisi kuwa ameshajua kuwa anahusika na balaa linaloendelea Arusha.
Baada ya kufikiri kwa kina Jacob Matata akaonelea ampigie simu ili amwambie kuwa hakuwa tayari kuonana na yeye na wala asingependa mzee huyo aendelee na tabia ya kumfuatafuata. Alichukua tena simu yake, ili kwa kutumia namba alizokuwa amepigiwa aweze kumpigia mzee huyo na ‘kumchimba mkwara mzito’. Alianza kuangalia orodha ya simu alizokuwa amepokea siku hiyo. Alisonya kwa nguvu pale alipofikia ilipokuwa namba ya simu aliyokuwa amepigiwa na mzee Edson na kukutana na neno ‘number withheld’ ikimaanisha kuwa mpigaji alikuwa ameficha namba yake isijulikane na mpokeaji.
.
Baada ya kujiuliza kwa upya akaazimia kuitikia wito wa mzee Edson na wakionana ndipo amweleze kuwa si salama kwake kujiingiza kwenye kisa hicho. Hata kama angekuwa na hatari, hatari ndio ilikuwa kazi yake na kitendo cha kukubali kuja Arusha ilimaanisha kuwa alikuwa tayari kukutana na hatari kama hizi. Hivyo ingekuwa ni ujinga kuogopa hatari wakati alikuwa amekuja kwenye hatari. Kwa hadhali kubwa aliadhimia kwenda kumsikiliza mzee Edson. Alichukua bastola yake ‘Automatic’ iliyotengenezwa Urusi na kuificha kati ya moja ya mifuko yake ya siri.
Wakati Jacob akiwa anataka kutoka chumbani humo ili kwenda kuonana na Mzee Edson, mara mlango wa chumba chake uligongwa!
Kabla hata hajafikiria nini cha kujibu au kufanya, mlango ulifunguliwa na mtu akaingia. Alipoingia tu tayari bastola ya Jacob Matata ilikuwa usawa wa paji la uso wa jamaa huyo.
“Karibu ndani na uketi huku mikono yako ikiwa imewekwa juu, ukishindwa kufanya hivyo ni imani yangu kuwa hutanilaumu kwa lile nitakaloamua kukufanya” Jacob alisema huku akitumia mguu wake kuusukuma mlango wa chumba hicho ambao ulitii na kujifunga.
Sura ya mtu huyu haikuwa ngeni sana kwa Jacob japo ilikuwa na mabadiliko madogo. Lakini aliweza kutambua kuwa alikuwa ni yule mzee aliyembeba kwenye gari lake jana toka uwanja wa ndege alipowasili Arusha.
Jambo moja bado lilikuwa linamtatiza Jacob kuhusu huyu mzee, kama ilivyokuwa jana alipokuwa ndani ya gari yake. Mzee huyu tabasamu fulani lilikuwa liko usoni kwake. Pamoja na kuwa bastola ya Jacob ilikuwa usawa wa uso wake lakini hakuonyesha hata chepe ya wasiwasi. Alitembea mpaka kwenye kochi lililokuwa chumbani humo na kukaa juu yake. Aliweka chini mkoba aliokuwa amekuja nao.
“Bwana Jacob najua kuwa umepata wito huko nje kwa hivyo sitakuwa na muda wa kupoteza zaidi. Ila nimeshataarifiwa kuwa kazi na safari hii ya kuja Arusha haikuwa katika mpangilio wako. Lakini kwa vile wewe ni mzalendo na mtanzania wa vitendo ndio maana umekubali kukatiza likizo yako na kuja kufanya kazi hii ya kusambaratisha kikundi hiki kinachotishia watu wasifanye yaliyo mema kwa Afrika” Aliongea mzee huyu katika sauti ya utulivu huku macho yake yakiwa sambamba na yale ya Jacob. Macho yake yalionyesha kitu fulani. Kitu hicho kilitambulika kwa Jacob kuwa mzee huyu alikuwa ni ‘mzee wa kazi’ aliyeiva sawasawa.
“Nimekuja hapa kwa ajili ya mambo matatu” aliendelea “moja; naamini kabla hujaondoka Dar Bi. Anita alikutaarifu juu ya mtu aliyemteua kukupa msaada pale utakapohitaji. Basi mtu huyo ndiye mimi.
Jambo la pili ni kukuhadhali kuwa watu hawa tayari wana taarifa juu ya uteuzi huu na wameshajua kuwa umeshaingia Arusha. Kama unakumbuka jana wakati nimekuja kukupokea walijaribu kutufuatilia bila mafanikio. Hii inaonyesha kuwa kuna mtu tayari ameshavujisha habari juu yako.
Tatu; Bi. Anita ameniagiza kukuletea vifaa ambavyo anaamini kuwa vinaweza kukusaidia katika kuendesha shughuli hii. Na ningekushauri kwa sasa kabla ya kutoka humu chumbani ujaribu kujibadilisha sura kwani unatafutwa sana na hawa watu” Alipomaliza kusema hayo Mzee huyo alimkabidhi Jacob mkoba mmoja mdogo uliokuwa umesheeni vitu mbalimbali vya kipelelezi. Jacob alivipokea huku akiwa bado ameshikilia bastola yake, hakuwa tayari kumwamini yeyote kwenye mazingira na wakati kama huo.
“Najua una hamu ya kujua mimi ni nani, lakini naona huu si muda muafaka wa kuongelea hilo. Ila utakapokuwa unanihitaji namba zangu za simu ni hizi hapa na mara kwa mara nitakuwa naegesha gari langu aina ya caldina ya rangi nyekundu pale Phillips jirani na zilipo ofisi za Pan African Movement. Mara zote nitakuwa hapo kwa ajili yako, mpaka hapo kazi hii itakapokuwa imekamilika. Pia nimeandaa nyumba ambayo unaweza kuifanya kama kambi yako ya mapumziko, hivyo unaweza kuniona na nikakuonyesha nyumba hiyo. Nakutakia mafanikio katika kazi ya hatari na ngumu iliyoko mbele yako, ila uwe makini ukijua fika kuwa adui yako anajua uwezo wako na anajua kuwa tayari uko Arusha. Wasingependa uendelee kuwa hai, ili yale waliyoazimia kufanya yatimie”. Alisema maneno hayo huku akisimama tayari kwa kuondoka. Jacob alijikuta anakosa hata neno moja la kuuliza, badala yake akawa anamwangalia mzee huyu kama mtu aliye katika maono ya kushangaza kama yale ya Musa na kijiti kilichokuwa kikiwaka pasipo kuteketea.
Yule mgeni wa ajabu alipotoka nje ndipo Jacob akaanza kuangalia ndani ya mkoba aliokuwa ameachiwa ili kuona kulikuwa na nini ambacho angehitaji kukitumia kwa wakati huo. Aliviangalia vyote kwa makini. Kwa kutumia mbinu fulani na vifaa alivyokuwa ameletewa, baada ya muda mfupi tayari alikuwa ameshabadilisha sura yake kwa moja kati sura za bandia alizokuwa amezikuta katika mkoba huo.
Baada ya kuhakikisha kuwa alikuwa tayari kwa lolote ndipo akaona kuwa ulikuwa ni wakati muafaka wa kwenda kumwona mzee Edson ambaye bila shaka alikuwa bado akimsubiri nje ya hoteli hiyo. Hakujua kuwa ni kwa vipi watu hawa walikuwa wanajua juu ya nyendo zake kwa urahisi kiasi hicho.
Alifungua mlango wa chumba ili atoke, kisha akaufunga nyuma yake kabla ya kuanza kushuka ngazi kuelekea chini. Akili yake ilikuwa ikimnong’oneza kuwa kazi ndiyo ilikuwa inaanza.
Alipita eneo la mapokezi na kutokezea sehemu iliyokuwa na mgahawa. Hapo ndipo akakumbuka kuwa alikuwa hajapata kifungua kinywa. Akaona ni bora akamwone mzee Edson na kumwambia kuwa amsubiri ili apate kifungua kinywa au kama na yeye alikuwa hajapata basi wapate kwa pamoja.
Jacob Matata tayari alikuwa ameshafika nje ya hoteli na kuanza kuelekea ilipokuwa sehemu ya kuegeshea magari ya wateja au wahusika wa hoteli. Aliangaza macho yake sehemu hiyo, akaiona gari aliyokuwa ameelekezwa na mzee Edson.
Wakati anapiga hatua kuelekea mahali ilipokuwa gari hiyo, Jacob hakuamini macho yake pale alipoona gari ya mzee Edson ikisambazwa vipande vipande. Ndiyo!! alikuwa ameona vizuri. Lile gari alilokuwemo mzee Edson lilikuwa limeshambuliwa na bomu. Wakati Jacob akiwa bado anafikiri nini cha kufanya mara akasikia mlio wa gari ikiondoka kwa kasi katika eneo hilo la hoteli na kuacha gari ya mzee Edson ikiwa inateketea vibaya. Alihisi kuwa gari hiyo iliyoondoka kwa kasi, ambayo hata hivyo hakufanikiwa kuiona ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na waliofanya shambulio hilo.

ITAENDELEA……….
No comments:
Post a Comment