Ads Here

Thursday, September 26, 2019

:MTEGO WA BOSS LADY. SEHEMU YA MWISHO.

WIKI MBILI BAADAE-BARABARANI.
Gari aina ya Toyota Prado nyeupe inaenda kwa mwendo wa wastani, ndani yupo Doni na Adela, “ulisema una jambo unataka kuniambia?” anasema Adela, Dino anabaki kimya kwa muda akionekana kama Mtu anayejishauri nini cha kusema, “ndio..nilitaka nikwambie kuwa..nashukuru kwa misaada yako..lakini sipo tayari kuendelea na haya maisha na wewe”, anasema Dino kwa kusita sita huku Adela akitoa headphone masikioni kwake, “sorry kuna kitu nilikuwa nasikiliza sijakusikia” anasema Adela, “nilikuwa nasema..” anasema Dino na mara anakatishwa na muito wa simu ya Adela, “sorry” anasema Adela huku akibofya simu na kuiweka sikioni.
Safari inandelea huku Adela akiwa mkono mmoja kwenye simu sikioni na mkono mwingine kwenye usukani, huku akiwa amezama kwenye maongezi akitumia lugha ya kiingereza, Gari linafika nje ya geti moja maridadi lenye nakshi za kuvutia, honi inapigwa na geti linafunguliwa na Gumbi, bwana anayeonekana kama ndiye Muangalizi wa nyumba ile.

NYUMBA YA KIFAHARI.
Gari linaingia na kusimama mbele ya nyumba ile nzuri ya kifahari, Adela na Dino wanateremka huku bado Adela akiwa na simu yake sikioni, Gumbi anakuja pale huku akimpatia Adela ufunguo wa nyumba, Doni anashtuka baada ya kumuona Gumbi, anamuangalia Gumbi kwa muda, picha inamjia kichwani huku kumbukumbu ya matukio kadhaa ya kukimbizana na Mgambo mitaani akimjia, Gumbi ni mmoja wa Wagambo ambao wamekuwa wanamsumbua mtaani, wakati huo Adela bado akiwa na simu sikioni akiongea, anaelekea kwenye ile nyumba na kufungua mlango wa nyumba ile na kuingia, “naona umachinga umeacha?” Gumbi anamuuliza Dino,Dino anabaki akimshangaa Gumbi bila kumjibu, huku Gumbi akitoa tabasamu lisiloonyesha uhalisia kama anamaanisha au anakebehi kwa swali lile, “njooni”, Doni na Gumbi wanashtushwa na wito wa Adela anayetokea ndani ya nyumba na kuelekea upande mwingine wa nyumba, Doni na Gumbi wanamfuata na kufika alipo, “funua” anasema Adela na kumfanya Gumbi mara moja na kwa haraka kufunua turubai lililopo pale na kuonekana Gari ndogo aina ya IST nyeupe, ambayo bado haina namba za usajili. “this is yours” Adela anamwambia Dino na kumuacha Dino anang’aa macho,

“hii ni gari yako” Adela anarudia maneno yale kwa Kiswahili, “alafu ukaanze kozi ya kiingereza ili tuende sambamba” anasema Adela huku akifungua mlango wa Gari ile, “ingia upige moto” Adela anamwambia Dino huku akimpatia ufunguo, Dino anapokea ufunguo na kuingia, anaingiza ufunguo na kupiga moto, “ni gari ya kazi sio ya kula bata na wenzako” anasema Adela, hali inayomfanya Dino muda huu wote kuachama mdomo kwa tabasamu lisilotoa muelekeo kama anashukuru ama tu haamini kile kinachotokea wakati ule, “mimi nasafiri kesho kutwa ila kuna Mtu anamalizia usajili atakuletea nyaraka zote za gari uanze kutumia” anasema Adela, “na litakuwa kwa jina lako”, anaongeza Adela na mara simu inaita, anaiweka sikioni na kusogea hatua kadhaa kutoka pale na kuanza kuongea, “umeshauchinja dogo” anasema Gumbi na kumfanya Dino kugeuka kumuangalia, “ukiwa na bosi utakula na kusaza” anasema Gumbi, “unaona hili jumba?” Gumbo anaendelea kumwambia Dino, “kule Njiro ipo kubwa ya hii” anasema Gumbi na mara anashtuka kumuona Adela anakuja, “haya zima gari twende” anasema Adela, Dino anazima gari na kutoka, anafunga mlango na kumpa Adela ufunguo, Adela anapokea anampa Gumbi ufunguo ule, “funika” Adela anamwambia Gumbi, kisha anaelekea kwenye Prado akifuatwa na Dino nyuma, wanaingia kwenye gari na Adela anawasha gari, “nyumba nzuri” anasema Dino na kumfanya Adela kutoa tabasamu jepesi, “naondoka jumatano kwenda Belgium..kama unadhani umeona nyumba ngoja utakapokuja Belgium uone nyumba” anasema Adela huku akiwa makini akirudisha gari nyuma, “kuna jambo ulikuwa unaniambia wakati tunakuja” anasema Adela huku akibadili gia kwenda mbele na kutoka pale getini, Dino anabaki kimya kwa muda, “sio jambo la haraka sana” anasema Dino, “Ok” anasema Adela huku gari likiongeza mwendo.

SIKU MBILI BAADAE-MGAHAWA WA UZUNGUNI-NJE.
Dino anafika alipoketi Bello, kijana Mtanashati, anayekaribia miaka 30 hivi, “karibu dogo” anasema Bello huku akiinuka na kuvua miwani nyeusi aliyovaa, na kumpa Dino mkono, “ahsante” anaitikia Dino huku akiketi, “kazi yako tayari” anasema Bello huku akifungua Mkoba wake, “kadi ya gari..leseni..na pass port” anasema Bello huku akitoa nyaraka moja baada ya nyingine na kuziweka pale mezani mbele ya Dino, Dino anaangalia nyaraka moja baada ya nyingine huku akionekana kushikwa butwaa, “safari ni wiki ijayo” anasema Bello, “aliniambia tutakuwa wawili” anasema Dino, “ilikuwa tuende wote..ila utatangulia mimi nitakuja baadae” anasema Bello, “kwa sasa tunaenda shopping..unahitaji mabegi” anasema Bello huku akiinuka pale kwenye kiti, Dino anakusanya nyaraka zake pale mezani na kuinuka, wanaondoka na kuelekea ilipo gari aina ya Subaru nyeusi, wanaingia na kuondoka.

UWANJA WA NDEGE WA KIA-WIKI MOJA BAADAE.
Dino ameketi sehemu ya abiria wanaosubiria kuingia kwenye Ndege, akiwa na simu akibofya bofya na headphones zikiwa masikioni, wanakuja Maofisa wawili, wanampa ishara ya atoe zile headphones masikioni, anazitoa, “tunamazungumzo na wewe kijana” anasema Ofisa mmoja na kumfanya Dino kukodoa macho kwa mshtuko, “inuka twende ofisini” anasema Ofisa Mwingine huku akimuonyesha kitambulisho chake, Dino na anainuka, “beba kila kitu chako” anasema Ofisa mmoja, Dino anabeba begi lake la mkononi, simu na jaketi na kufuatana na Maofisa wale.

MWAKA MMOJA BAAAE-NYUMBANI KWA DINO.
Dino akionekana amedhoofu na sura kuchoka, ameketi kitandani, Tula yupo pembeni akitumia kitambaa anachochovya kwenye bakuli liliopo juu ya meza na kumkanda Dino mgongoni, huku Dino akikunja uso kuonyesha anahisi maumivu, “hii dawa inauma mpaka nasikia kizunguzungu” anasema Dino, “vumilia” anasema Tula, wanabaki kimya kwa muda, “sikujua kama dada mrembo vile anaweza kufanya mambo kama yale”, anasema Dino kwa sauti ya chini na kwa hisia, “kwa maisha ya kifahari kama yale Dino ulipaswa ujiulize mara mbili”, anasema Tula huku akiendelea na zoezi lile la kumkanda, “sikujua kama moja ya mabegi niliyokuwa nayo pale uwanjani lilikuwa na madawa ndani” anasema Dino, “siku zote tamaa mbele mauti nyuma Dino” anasema Tula, “tamaa ndio ilikuponza”, anaongeza Tula, wanabaki kimya kwa sekunde kadhaa huku zoezi la kukanda linaendelea, “sidhani kama huko ulikuwa unaoga Dino..mwaka mmoja tu upele hivi..je ungemaliza hiyo miaka yote saba?” anasema Tula huku akimaliza zoezi lile la kumkanda Dino mgongoni, “tumshukuru Mungu kwa kila jambo Tula” anasema Dino, “sasa kifuatacho Dino ni kwenda kupima”, anasema Tula na kumfanya Dino ashtuke na kumuangalia Tula, “kwa nini unasema hivyo?” anauliza Dino kwa mshangao, “kwa haya uliyopitia mwaka mzima” anasema Tula, “Tula kama unafuatilia zile stori za vijiweni kuhusu jela ..naomba nikwambie kuwa sijaguswa” anasema Dino, “mimi sipo huko Dino” anasema Tula, kinapita kimya kifupi, “tuachane na hizo stori Tula..siendi kupima full stop” anasema Dino, “tuongee kuhusu maendeleo yako” anasema Dino, “niambie kama ule mtihani ulifanikiwa kufanya” anauliza Dino, “niliongea na Mkuu wa chuo..nikafanya mtihani nikalipa baadae kidogokidogo na nilifanikiwa kupata kazi pale pale Hotelini nilipokuwa nafanya Mafunzo kwa vitendo” anaongeza Tula, kinapita kimya kifupi, “kuna moja bado nasubiri kusikia Tula” anasema Dino, “kuhusu nini Dino?” anauliza Tula, “kuhusu..hatma ya mimi na wewe?” anasema Dino, Tula anashusha pumzi, “Dino..najua nitakukwaza kwa hili” anasema Tula na kumfanya Dino kuonyesha mshtuko usoni, “mimi nilishachukua muelekeo mwingine wa maisha yangu” anasema Tula, “una maana gani Tula?” anauliza Dino kwa sauti iliyokata tamaa, “mimi tayari nina Mtu mwingine kwa sasa” anasema Tula na kumfanya Dino kukodoa macho, “sidhani kama unamaanisha hicho unachoongea Tula” anasema Dino kwa sauti inayotetema, “hebu na wewe vaa viatu vyangu Dino” anasema Tula, “ulihukumiwa jela miaka saba..nani angejua kama ungetoka baada ya mwaka mmoja kwa msamaha wa Raisi” anasema Tula, “Tula” anasema Dino huku machoni akilengwa na machozi, “samahani Dino..sikudhamiria kukuumiza”, anasema Tula huku akimpatia Dino leso ya kufutia machozi, “am sorry Dino” anasema Tula kisha anainuka kutaka kutoka, “Tula” anaita Dino, Tula anatulia, “unaniacha kwenye wakati mgumu” anasema Dino, “pole” anasema Tula huku akishika kitasa kutaka kufungua mlango, “Tula unaondoka..hatujamaliza maongezi” anasema Dino, Tula anabaki kimya kwa muda, anageuka na kushusha pumzi nzito, “tufanye hivi Dino” anasema Tula, “kama kuna lolote la kuongea..tutaongea ukishapima afya” anasema Tula na kumfanya Dino ainuke pale kitandani, “vipi?” anauliza Tula akimshangaa Dino kuinuka, “twende tukapime” anasema Dino, “sio sasa hivi Dino” anasema Tula huku akimkalisha Dino pale kitandani, “tutaenda kesho..mimi muda huu naingia kazini” anasema Tula, “sawa..kesho nitakusubiri asubuhi” anasema Dino, Tula anafungua mlango na kutoka.

MIEZI MINNE BAADAE-HOTELI YA MOUNT MERU-NJE BUSTANINI.
Tula, Dino na Watu kadhaa, Dino anamvisha Tula pete huku akishangiliwa na Wenzao wale, kisha kila mmoja anamkumbatia Dino na Tula mmoja baada ya mwingine, huku wakiendelea na vinywaji na vitafunwa vilivyo kwenye meza iliyo pembeni, wakisindikizwa na muziki laini unaotoka kwenye spika pembeni.


MWISHO.

No comments:

Post a Comment

Chombezo : Penzi La Shemeji Sehemu Ya Pili (2)

Nilishtuka na kutaka kukimbia ila shemeji akanishika mkono "Unakimbia nini?" aliuliza " Hapana sikimbii" nikamjibu ...