Ads Here

Thursday, September 26, 2019

MTEGO WA BOSS LADY. SEHEMU TA PILI.

NYUMBANI KWA DINO-NDANI-ASUBUHI.
Dino ameketi juu ya kitanda akifunga kamba za viatu, anainuka na kuchukua jaketi lilotundikwa ukutani, anavaa na kutoka.

NYUMBANI KWA DINO-NJE.
Dino anatoka, anakwenda kwa hatua kadhaa, anafika kwenye kona anamkuta Tula amesimama sambamba na ukuta wa moja ya nyumba, “kuna tatizo gani Dino hupatikani?” Tula anauliza mara tu baada ya Dino kufika pale aliposimama, “nimeibiwa simu” anasema Dino, “ooh..pole” anasema Tula kwa sauti ya huruma, “na ile hela vipi nikalipe?” anauliza Tula, Dino anabaki kimya kwa muda “sijui hata nikwambie nini Tula” anasema Dino na kumuacha Tula amezubaa, “kwa nini usijaribu kuongea na bosi wako akupe ufanye mtihani tumrudishie” anasema Dino, “pesa ya mtihani alinipa nikamtumia mdogo wangu Mgonjwa kijijini..na si nilikwambia” anasema Tula, “ada yote amelipa yeye nilidhani si vizuri nianze tena kumsumbua” anasema Tula na kumfanya Dino kubaki kimya kwa sekunde kadhaa, “hebu vuta subira kuna pesa natarajia kuipata kabla ya jioni” anasema Dino, Tula anashusha pumzi, “jitahidi basi Dino dear” anasema Tula kisha anambusu Dino shavuni na kuondoka, “masomo mema” anasema Dino.

NYUMBANI KWA ADELA-NYUMBA NZURI NA YA KIFAHARI-NDANI.
Dino ameketi kochini akiangalia TV, akiwa na muonekano tofauti, nguo alizovaa zimempendeza vilivyo, ndani pale kumesheheni samani nzuri za kupendeza na za gharama kubwa, anakuja Adela akiwa na glasi mbili na chupa ya mvinyo mwekundu,”huu sasa ndio muonekano ninaotaka uwe nao siku zote”, anasema Adela akiwa amesimama mbele ya Dino, kisha anaziweka glasi mezani “ila mimi situmii pombe dada” anasema Dino, “hii sio pombe acha ushamba” anasema Adela huku akiifungua ile chupa na kumimina mvinyo kwenye zile glasi, “si unajua kuendesha gari?” anauliza Adela,Dino anabaki kimya kwa muda kama aliyeshtushwa na swali lile, “lakini sina leseni” anasema Dino, “hiyo ni kazi ndogo” anasema Adela huku akiketi pale kwenye kochi, anachukua remote mezani na kuibofya kubadilisha kinachoonekana kwenye ile flat TV kubwa iliyopo mbele ukutani, “ulisema unapenda movies?” anauliza Adela, “ndio” anajibu Dino ambaye bado anaonyesha hali ya ugeni ndani pale, “jisikie upo nyumbani” anasema Adela baada ya kumaliza zoezi la kusaka channel kwenye TV.

NYUMBANI KWA DINO-ASUBUHI.
Tula anafika na kugonga mlango mara kadhaa, “Doni hayupo” Tula anashtushwa na sauti ya Dada Jirani aliyekuja nyuma yake, “habari yako” anasalimu Tula, “nzuri..Doni sijamuona tangu jana” anasema Dada Jirani na kupelekea Tula kubaki ameduwaa, “basi akija naomba umwambie Tula alifika” anasema Tula, “sawa nitamwambia” anasema Dada Jirani, Tula akiondoka.

HOTELINI NDANI-MCHANA.
Tula akiwa amevaa sare maridadi za Wahudumu wa hoteli, akiwa na kijitabu kidogo mkononi na kalamu anaenda walipoketi Wageni wawili, mara Tula anashtuka kumuona Dino ndiye mmoja wa Wageni wale wawili, Dino naye anainua macho na kukutana macho kwa macho na Tula, Dino anapatwa na mshtuko mithili ya mtu aliyechomwa sindano mgongoni, wote wanabaki wanashangaana, Adela bado yupo makini akisoma kitabu chenye orodha ya vyakula na vinywaji almaarufu kama menu, anainua kichwa na kumuona Doni amezubaa, “nini”, anauliza Adela, “sio kitu” anasema Doni, “karibuni..mtatumia nini?” anauliza Tula haraka haraka kumkatisha Adela, huku akiweka kitabu chake na kalamu tayari kuandika wanachoagiza Wageni wake, “hebu tupe muda kidogo tujadiliane alafu tutakuita” anasema Adela, Tula anaondoka, “hivi ndio tutakuwa tunaishi siku zote”, anasema Adela, “pale kwangu huwa sipiki” anaongeza Adela, “ni gharama”, anasema Dino, “ni gharama kama utalipa wewe..kwangu sio gharama” anasema Adela, “leo unataka kula nini?” anauliza Adela,Dino anabaki amezubaa kwa sekunde kadhaa, “naomba uniagizie tu chochote mimi nitakula” anasema Dino na kumfanya Adela aangue kicheko laini hadi kuinamisha kichwa, “any way..utazoea tu” anasema Adela, “binti njoo” Adela anamuita Tula.

NYUMBANI KWA DINO-NDANI.
Dino ameketi kwenye kitanda amejiinamia, huku Tula akiwa amesimama mlangoni akiwa amekunja mikono yake kifuani, “sioni kama unachoongea kina ukweli Dino” anasema Tula kwa sauti ya chini na ya upole, “huo ndio ukweli Tula” anasema Dino, “nilienda kuomba mkopo..akanialika chakula..nisingeweza kukataa”, anasema Dino, “mbona hukuniambia kabla kama unaenda kwenye chakula na Mtu” anauliza Tula, “na ungejua kama mafunzo yangu kwa vitendo nafanyia kwenye Hoteli ile usingekubali kuja pale Dino”, anaongeza Tula huku Dino amebaki kimya amejiinamia, “najua nimekosea lakini hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na yule Dada Tula”, Dino anasema, “sio kwa kubadilika hivyo Dino” anasema Tula, “nguo mpya..viatu..simu mpya..mawasiliano umekata” Tula anaendelea kusema, “ni nani utamdanganya kama Mtoto Dino” anaongeza Tula kwa maneno yaliyojaa hisia kali na kuvunjika moyo.

Wanabaki kimya kwa muda, Dino anashusha pumzi, “kilichotokea kimetokea Tula..naomba tuanze ukurasa mpya” anasema Dino, “hapana Dino naomba tu nikuachie uhuru uendelee na maisha yako uliyochagua” anasema Tula na kufungua mlango na kutoka, “Tula” anaita Dino huku anainuka na kumfuata Tula, “kwa heri Dino” anasema Tula huku akiondoka, Dino anabaki amesimama pale mlangoni akimsindikiza kwa macho, Dino anaufunga mlango na kurudi kuketi pale kitandani akionekankama Mtu aliyebeba mzigo mzito kichwani kwake.

No comments:

Post a Comment

Chombezo : Penzi La Shemeji Sehemu Ya Pili (2)

Nilishtuka na kutaka kukimbia ila shemeji akanishika mkono "Unakimbia nini?" aliuliza " Hapana sikimbii" nikamjibu ...